mateoshija
mateoshija
Untitled
253 posts
Don't wanna be here? Send us removal request.
mateoshija · 2 months ago
Text
Dominika ya PASAKA- ALELUYA BWANA AMEFUFUKA, KWELI KWELI AMEFUFUKA
Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, tutashangilia na kuifurahia. Leo ni kilele cha imani ya Kikristo – Yesu amefufuka! Sio siku ya huzuni, bali ya furaha isiyo na kifani. Kwaresma imeisha, sasa tunaanza kipindi cha siku 50 za Pasaka kinachomalizika kwa Pentekoste. Leo ni siku ya kusherehekea kwa heshima: fanya sherehe nyumbani, shiriki Misa, na tangaza furaha ya Kristo aliye hai. Sala za Furaha…
0 notes
mateoshija · 2 months ago
Text
Kwaresma Siku ya 46-JUMAMOSI KUU: Subiri kwa Kimya na Tumaini
Mpendwa, Jumamosi Kuu ni siku ya kimya na matumaini, tukitafakari Yesu akiwa kaburini. Ni siku pekee ambapo hakuna Misa wala ibada hadi usiku wa Kesha ya Pasaka, hivyo waamini wanahimizwa kudumisha hali ya toba, sala, na kutafakari fumbo la Msalaba hadi Ufufuko. Wengine huendelea na funga ya hiari kama sadaka ya kiroho hadi usiku. Leo tunaendelea na Novena ya Huruma ya Mungu (siku ya pili) kwa…
0 notes
mateoshija · 2 months ago
Text
Kwaresma Siku ya 45-IJUMAA KUU: Tafakari, Funga, na Tenda Huruma
Mpendwa Tumefikia Kilele cha Kwaresma Yetu Leo ni Ijumaa Kuu, siku takatifu ya huzuni na sala duniani kote. Siku hii tunaungana na mateso ya Yesu kwa kufunga, kutotumia nyama, na kujinyima anasa. Tunahimizwa kuwa kimya, wenye unyenyekevu, na kutumia muda wa tafakari badala ya burudani au mitandao. Watoto wanaweza kushiriki kwa kujinyima vitafunwa au michezo. Ibada ya jioni ni ya pekee, ikiwa…
0 notes
mateoshija · 2 months ago
Text
Kwaresma Siku ya 44-Alhamisi Kuu: Tumikia kwa Upendo Kama Yesu
Mpendwa, Leo ni Alhamisi Kuu, siku ambayo tunakumbuka matukio makubwa mawili: Karamu ya Mwisho ambapo Yesu alianzisha Ekaristi Takatifu na Daraja Takatifu (Upadre). Hii si siku ya kufunga chakula, bali ni siku ya kujinyima ubinafsi kwa kujitoa kwa huduma ya wengine – kama Yesu alivyowatumikia wanafunzi wake kwa kuwaosha miguu. Leo tunaalikwa kuishi upendo kwa vitendo: kuwasaidia familia zetu,…
0 notes
mateoshija · 2 months ago
Text
Kwaresma Siku ya 43: Jumatano ya Wiki Kuu - Usaliti wa Yuda: Jihoji, Tubu, na Kuwa Mwaminifu kwa Kristo
Mpendwa Leo, tunatafakari usaliti wa Yuda Iskariote (Mt 26:14-16). Tukiwa karibu tunaazna siku tatu kuu za mateso,  tunaalikwa kufunga si kwa chakula tu bali kwa hisia mbaya kama chuki, kinyongo, na tamaa ya fedha—vitu ambavyo vinaweza kutufanya tumsaliti Yesu. Tafakari, je, kuna mahali pa maisha yako ambapo umeweka faida au sifa mbele ya uaminifu kwa Mungu? Katika sala, tunahimizwa kuingia saa…
0 notes
mateoshija · 2 months ago
Text
Kwaresma Siku ya 42: Jumanne ya Wiki Kuu- Tii, Jinyime, Tenda kwa Upendo
Mpendwa , Tunapoikaribia zile siku tatu Kuu, leo tunakumbushwa kwamba kufa kwa ubinafsi ndiko kunakotoa uzima wa kiroho. Yesu alijinyenyekeza na kuwa mtii hadi kifo cha msalaba (Wafilipi 2:8). Leo unatakiwa kuchukua hatua ya kujikana kwa vitendo—jinyime haki yako ya mwisho katika mabishano, acha tamaa au starehe inayokufunga kiroho. Kwa kufanya hivyo, unashiriki mfano wa Kristo ambaye…
0 notes
mateoshija · 2 months ago
Text
Kwaresma Siku ya 41 - Jumatatu ya Wiki Kuu: Toba ya Kweli Inafungua Mlango wa Pasaka
Mafundisho ya leo yanahimiza maandalizi ya ndani kabla ya Alhamisi Kuu kwa kufanya funga yenye lengo la toba na upatanisho. Waamini wanahimizwa kujinyima starehe kama vile TV au mitandao, kuchunguza dhamiri kwa kutumia Amri 10 za Mungu, na kuandika dhambi walizotenda kwa ajili ya ungamo. Funga hii inalenga kujipamba kiroho kwa toba kama waalikwa wa harusi. Sala ya Zaburi 51 na Zaburi 139 inafaa…
0 notes
mateoshija · 2 months ago
Text
Dominika ya Matawi (Dominika ya Mateso ya Bwana): Anza Wiki Kuu kwa Unyenyekevu na Toba ya Dhati
Ndugu Mpendwa Dominika ya Matawi inaashiria mwanzo wa Wiki Kuu, na waamini wanahimizwa kuingia kipindi hiki kwa unyenyekevu na moyo wa toba. Ingawa si siku rasmi ya kufunga, tunashauriwa kufanya funga ya moyo kwa kujinyima maneno yasiyo ya lazima, malalamiko, na anasa, ili kujitakasa kwa ajili ya mateso ya Kristo. Tunamkumbuka Yesu akiingia Yerusalemu kwa unyenyekevu, akiwa juu ya punda,…
0 notes
mateoshija · 2 months ago
Text
WIKI KUU - HOLY WEEK
Wiki Kuu, Tunafanya kumbukumbu ya upendo mkuu wa Mungu kwetu kupitia mateso, kifo, na ufufuko wake.-Ni wiki ya kujitahidi kuwa katika utakatifu DOMINIKA YA MATAWIYesu anaingia Yerusalemu kwa shangwe. Mathayo 21:1-11 JUMATATU KUUMaria ampaka Yesu marashi. Yuda anaghadhabika na kuondoka. Yohana12:1-11 JUMANNE KUUYesu anatabiri usaliti wa Yuda na Petro kumkana mara tatu. Yohana 13:21-38 JUMATANO…
0 notes
mateoshija · 2 months ago
Text
Kwaresma  Siku ya 39: Jitakase Kabla ya Wiki Kuu
Wapendwa, Tunaopelekea Wiki Kuu, na mafundisho yanatualika kufunga kwa nia ya kujitakasa kiroho ili kumpokea Kristo kwa moyo safi. Waamini wanahimizwa kujinyima chakula au starehe wanazozipenda sana, na kutumia muda huo kufanya tafakari ya kina, kuchunguza dhamiri kwa kutumia Amri za Mungu, na kuandika dhambi zao kwa ajili ya maandalizi ya kitubio. Sala ya leo inalenga kuomba uamsho wa ndani wa…
0 notes
mateoshija · 3 months ago
Text
Kwaresma Siku ya 38 : Jinyime kwa Ajili ya Wale Wasioamini
Mpendwa, Mafundisho ya leo yanahimiza waamini kufunga kwa nia ya kuombea wale waliopoteza imani au hawamjui Mungu kabisa. Kwa kujinyima mlo au starehe fulani, tunashiriki katika kazi ya ukombozi wa Mungu kwa niaba ya wengine. Hii ni sadaka ya upendo yenye nguvu ya kiroho. Katika sala, tunahimizwa kumwomba Mungu atupatie mioyo laini na roho ya kutii, tukitafakari maneno kutoka Ezekieli 36:26.…
0 notes
mateoshija · 3 months ago
Text
Kwaresma Siku ya 37 : Jinyime Kwa Ajili ya Kuwa Karibu Zaidi na Yesu
Mpenda, Karibu Mafundisho ya leo yanatualika kufunga kwa namna ya kiroho kwa kujinyima si tu chakula, bali pia maneno yasiyo ya lazima, malalamiko, na majivuno. Lengo ni kujiunganisha kwa undani na mateso ya Kristo anayekaribia kuingia katika mateso ya Pasaka. Kama Yesu alivyonyamaza mbele ya washtaki wake, waamini wanahimizwa kufanya funga ya kimya na utulivu wa moyo. Katika sala, tunaalikwa…
0 notes
mateoshija · 3 months ago
Text
Kwaresma ya Siku ya 36 : Jifunze Kukubali Mapenzi ya Mungu kwa Utulivu
Mpendwa , Karibu tena kwa tafakari hii ya Kwaresma Mafundisho ya leo yanahimiza kufunga kwa moyo wa unyenyekevu, kwa nia ya kukubali mapenzi ya Mungu hata katika hali zisizopendeza. Funga hii inalenga kuacha kutaka mambo yaende kwa namna yetu na badala yake tujifunze kutulia na kuamini mpango wa Mungu. Sala ya leo inasisitiza utulivu wa ndani na kumwomba Yesu atufundishe kutii kama Yeye…
0 notes
mateoshija · 3 months ago
Text
Kwaresma Siku ya 29 : Jinyime kwa Ajili ya Kuokoa Nafsi
Siku ya Leo ya Kwaresma inalenga kufunga kwa nia ya kuombea wokovu wa nafsi moja – mtu wa familia, rafiki au yeyote aliye mbali na Mungu. Funga hii si kwa desturi, bali kwa upendo, ukijinyima kwa ajili ya wokovu wa wengine. Katika sala, waamini wanahimizwa kusali Koronini ya Huruma ya Mungu na Zaburi 103, wakimwomba Mungu awahurumie wale waliopotoka. Tafakari ya Injili ya Yohana 8:1–11…
0 notes
mateoshija · 3 months ago
Text
Kwaresma Siku ya 28 : Tafuta Utulivu wa Ndani kwa Kujinyima Kelele za Dunia
Leo ni fursa ya kipekee ya kufanya funga ya utulivu wa moyo. Badala ya kujinyima chakula tu, jinyime pia kelele na shughuli zisizokuwa za lazima—hasa zile zinazokusababisha kuishi kwa mazoea bila tafakari. Zima simu kwa muda fulani, epuka mitandao ya kijamii, zuia mazungumzo yasiyo ya lazima. Tumia muda huo kutafakari maisha yako, hususan maeneo ambayo bado yanahitaji toba ya kweli. Funga hii ni…
0 notes
mateoshija · 3 months ago
Text
Dominika 5 Kwaresima: Mwenyezi Mungu anatuhurumia sisi wadhambi, anatuahidia maisha mapya.
Wapendwa leo nawkaribisha tutafakari pamoja kuwa “Mwenyezi Mungu anatuhurumia sisi wadhambi, anatuahidia maisha mapya”. tafakari hii inapatika hapa basi tushiriki pamoja . Shukrani kwa Padre Bonaventura Maro, C.PP.S., Kolleg St. Josef, Salzburg, Austria aliyetoa Tafakari hii.
0 notes
mateoshija · 3 months ago
Text
Kwaresma Siky ya 32 : Mfuate Kristo Katika Maisha ya Kila Siku
Ndugu mpendwa katika Kristo, Katika safari yetu ya Kwaresma, tunajifunza kwamba kumfuata Kristo kunahitaji uaminifu na kujitoa katika maisha yetu ya kila siku, hata katika mambo madogo. Mpendwa, Injili ya Yohana 21:1-14, inatueleza jinsi Yesu alivyowatokea wanafunzi wake baada ya kufufuka kwake. Wanafunzi walikuwa wakivua samaki usiku kucha bila mafanikio. Asubuhi, Yesu aliwatokea na…
0 notes