Tumgik
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
Al-Ma'idah 5:39 فَمَن تَابَ مِنۢ بَعْدِ ظُلْمِهِۦ وَأَصْلَحَ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَتُوبُ عَلَيْهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ Lakini mwenye kutubia baada ya dhulma yake, na akatengenea, basi Mwenyezi Mungu atapokea toba yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu.
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
Al-Ma'idah 5:1 يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَوْفُوا۟ بِٱلْعُقُودِۚ أُحِلَّتْ لَكُم بَهِيمَةُ ٱلْأَنْعَٰمِ Enyi mlio amini! Timizeni ahadi.
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
We live and learn!! (at Arusha, Tanzania)
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
Wema NI Lugha ambayo kipofu anaweza kuiona na kiziwi kuiskia.
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
Msoko....No fagi...Acha kuendea...dau kumi. ..banju atutaki minyukwa tu...ukidead unatema...nikumbushe mengine ya kwenye msoko najua Manyugu wengi HUMu...
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
Madness is what you demonstrate And that's exactly how anger works and operates Man, you gotta have love just to set it straight Take control of your mind and meditate Let your soul gravitate to the love, y'all, y'all
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
Al-Ma'idah 5:2 يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تُحِلُّوا۟ شَعَٰٓئِرَ ٱللَّهِ وَلَا ٱلشَّهْرَ ٱلْحَرَامَ وَلَا ٱلْهَدْىَ وَلَا ٱلْقَلَٰٓئِدَ وَلَآ ءَآمِّينَ ٱلْبَيْتَ ٱلْحَرَامَ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّن رَّبِّهِمْ وَرِضْوَٰنًاۚ وَإِذَا حَلَلْتُمْ فَٱصْطَادُوا۟ۚ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَـَٔانُ قَوْمٍ أَن صَدُّوكُمْ عَنِ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ أَن تَعْتَدُواۘ وَتَعَاوَنُوا۟ عَلَى ٱلْبِرِّ وَٱلتَّقْوَىٰۖ وَلَا تَعَاوَنُوا۟ عَلَى ٱلْإِثْمِ وَٱلْعُدْوَٰنِۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ Enyi mlio amini! Msivunje hishima ya alama ya Dini ya Mwenyezi Mungu wala mwezi mtakatifu, wala wanyama wanao pelekwa Makka kuchinjwa, wala vigwe vyao, wala wanao elekea kwendea Nyumba Takatifu, wakitafuta fadhila na radhi za Mola wao Mlezi. Na mkisha toka Hija yenu basi windeni. Wala kuwachukia watu kwa kuwa wali- kuzuilieni kufika Msikiti mtakatifu kusikupelekeeni kuwafanyia uadui. Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
Al-Anfal 8:2 إِنَّمَا ٱلْمُؤْمِنُونَ ٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ ٱللَّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ ءَايَٰتُهُۥ زَادَتْهُمْ إِيمَٰنًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zake huwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi.
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
Yah Rabbi nistiri Mja wako..wastiri watoto wangu..wastiri wazazi wangu..mstiri Mke wangu..wastiri kaka zangu...wastiri dada zangu..wastiri Ndugu zangu...wastiri jamaa zangu..wastiri rafiki zangu..wastiri Ndugu zangu..wastiri jirani zangu..Yah Allah nakuomba uyaongoze makundi yote hayo katika njia iliyonyooka..Yah maalik uwakubali na uwaridhie kwani katika wao tumo wenye kutafuta radhi zako hivyo tunakuomba uturidhie..sote tunakosea hivyo utusamehe makosa Yetu..wapo waliopotea basi Allah tunakuomba uwarudishe..Hakuna mwenye uwezo wa kuvumilia adhabu zako hivyo utuokoe..yah arrahmani tuhurumie na utupe mafanikio hapa duniani,kaburini na kesho akhera...RABBANA AATINA FIIDUNIA YAAHASANA WAFIL AAKHERAT HASANA WAKINAADHABBANNAR..RABBI GHUFIRLAANA WARHAMNA ANTAMAULANA FAANSURNA ALALKAUMIL KAAFIRIIN...SUBHANAKA RABBIKA RABBIINZAT AAMMAYASWIFUN........malizia kwenye comment!!
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
Al-Kahf 18:16 وَإِذِ ٱعْتَزَلْتُمُوهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ إِلَّا ٱللَّهَ فَأْوُۥٓا۟ إِلَى ٱلْكَهْفِ يَنشُرْ لَكُمْ رَبُّكُم مِّن رَّحْمَتِهِۦ وَيُهَيِّئْ لَكُم مِّنْ أَمْرِكُم مِّرْفَقًا Na mkijitenga nao na vile wanavyo viabudu badala ya Mwenyezi Mungu, basi kimbilieni pangoni, akufungulieni Mola wenu Mlezi rehema yake, na akutengenezeeni ya kukufaeni katika mambo yenu.
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
Hud 11:18 وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًاۚ أُو۟لَٰٓئِكَ يُعْرَضُونَ عَلَىٰ رَبِّهِمْ وَيَقُولُ ٱلْأَشْهَٰدُ هَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ كَذَبُوا۟ عَلَىٰ رَبِّهِمْۚ أَلَا لَعْنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلظَّٰلِمِينَ Na nani aliye dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo? Hao watahudhurishwa mbele ya Mola wao Mlezi, na mashahidi watasema: Hawa ndio walio mtungia uwongo Mola wao Mlezi. Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate walio dhulumu,
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
Hud 11:15 مَن كَانَ يُرِيدُ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَٰلَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لَا يُبْخَسُونَ Wanao taka maisha ya dunia na pumbao lake tutawalipa humo vitendo vyao kaamili. Na wao humo hawatopunjwa.
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
Hud 11:4 إِلَى ٱللَّهِ مَرْجِعُكُمْۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ Marejeo yenu ni kwa Mwenyezi Mungu tu. Naye ni Muweza wa kila kitu.
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
Ujue kuna mambo mengine sio mpaka MTU akusimamie wala hayahitaji kufikiria saana..don't be a school boy...just think..
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
Al-Baqarah 2:22 ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُمُ ٱلْأَرْضَ فِرَٰشًا وَٱلسَّمَآءَ بِنَآءً وَأَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَأَخْرَجَ بِهِۦ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ رِزْقًا لَّكُمْۖ فَلَا تَجْعَلُوا۟ لِلَّهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ (Mwenyezi Mungu) ambaye amekufanyieni hii ardhi kuwa kama tandiko, na mbingu kama paa, na akateremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo akatoa matunda yawe riziki zenu. Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika, na hali nyinyi mnajua.
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
hizi pesa zinazotumika duniani kote zinazojulikana kama (Paper Money) ambazo zimebuniwa na kupewa thamani na watu kama sisi, Allah subhana uwataala hazitambui na NI haramu. kwa watu waliosoma Mambo ya elimu ya secular wanatambua haya hasa katika somo la international monetary economy NI KWAMBA maana ya pesa NI medium of exchange(kama alivyokipangia MTUME tende kwa tende au kipande cha silver au dhahabu kwa ngano...Maana yake ndani ya hizi pesa za watu hakuna uhadilifu na Kuna ufisad na Riba,mnamo mwaka 1933 marekani walishusha thamani ya dhahabu na kuwapora watu wote dhahabu kwa kuamuru kwamba yeyote mwenye dhahabu au silver arudishe kwenye fedaral reserve bank na asiyefanya hivyo Basi atapewa hukumu ya miaka kumi jela na kumpa kila mwenye kurudisha coin Moja ya dhahabu kwa dola 20 BAADA ya kuhakikisha kila MTU amerudisha dhahabu wakapandisha tena thamani ya dhahabu kwa dola 35 HAPO walifanya UFISADI na waliibia watu zaidi ya mamilioni ili kupinga pesa za anazozitambua Allah alizozilidhia Allah dhahabu na silver coins ambazo kiarabu NI dirham na dinar ambapo kipindi HICHO zilikuwa zikitumika...Maana ya pesa kidini lazma kwanza pesa yenyewe iwe na thamani yani thamani ya pesa iko ndani ya pesa yenyewe kwanza.. Sasa wewe jiulize iyo mibati na mikaratasi yenyewe kama yenyewe ina thamani ndani yake?? Lakini dhahabu na silver tayari Allah kishavipa thamani na hakuna anayeweza kutoa kopi au kufanya feki ya dhahabu Wala silver...Allah mwenyewe ndiye anaeshusha thamani ya dhahabu na silver na sio watu...Leo binaadamu ndiye anakupangia thamani...Yani anatengeneza karatasi na mibati alafu anatia namba tayari inakuwa pesa...Sasa Leo unaziona na kuzishika kesho plan yake NI kutengeneza pesa ambazo huwezi kuzigusa Wala kuziona ambapo ndiyo kubaya Zaid...Ukisoma historia hakuna MTUME yeyote aliyetumia huu ujinga hadi MTUME WA mwisho...Ndiyo maana MTUME akatoa mfano WA Riba itakavyojificha NI kama kidudu kidogo cheusi kilicho juu ya jiwe jeusi wakati WA usiku huwezi kuona mpaka uchunguze sana...Na Masheikh wetu maulamaa hawawezi kuona HAYA kwasababu hawajui history Wala hawana elimu ya haya mambo kwahiyo HAYA yote yamo ndani ya Quran yote hadi pesa anazozitaka Allah kazitaja
0 notes
ommarizo-blog · 7 years
Photo
Tumblr media
KWA JINA LA ALLAH MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 113. Na namna hivi tumeiteremsha Qur'ani kwa Kiarabu, na tumekariri humo maonyo ili wapate kuogopa na kujilinda na iwaletee makumbusho. 114. Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki. Wala usiifanyie haraka hii Qur'ani, kabla haujamalizika ufunuo wake. Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu. 115. Na hapo zamani tuliagana na Adam, lakini alisahau, wala hatukuona kwake azma kubwa. 116. Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam! Wakasujudu, isipo kuwa Iblisi, alikataa. 117. Tukasema: Ewe Adam! Hakika huyu ni adui yako na wa mkeo. Basi asikutoeni katika Bustani hii, mkaingia mashakani. 118. Hakika humo hutakuwa na njaa wala hutakuwa uchi. 119. Na hakika hutapata kiu humo wala hutapata joto. 120. Lakini Shet'ani alimtia wasiwasi, akamwambia: Ewe Adam! Nikujuulishe mti wa kuishi milele na ufalme usio koma? 121. Basi wakaula wote wawili, na uchi wao ukawadhihirikia na wakaanza kujibandika majani ya Bustani. Na Adam akamuasi Mola wake Mlezi, na akapotea njia. 122. Kisha Mola wake Mlezi akamteuwa, naye akamkubalia toba yake, naye akamwongoa. 123. Akasema: Ondokeni humu nyote, hali ya kuwa ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika. 124. Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu. 125. Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona? 126. (Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhaalika leo unasahauliwa. 127. Na hivi ndivyo tutakavyo mlipa kila apitaye kiasi, na asiye amini ishara za Mola wake Mlezi. Na hakika adhabu ya Akhera ni kali zaidi, na inadumu zaidi. 128. Je! Haikuwabainikia tu; vizazi vingapi tuliviangamiza kabla yao, nao wanatembea katika maskani zao? Hakika katika hayo ziko ishara kwa watu wenye akili.
0 notes