Don't wanna be here? Send us removal request.
Text
Umeshawahi kukumbwa na maradhi
Ama kuchapwa na vibaka wezi wa majambazi
Ukashindwa kufanya kazi ukaamua kuyahama yako makazi
Ukarudi nyumbani ili ukauguzwe na wako wazazi
Ukaharisha na kutapika ndani ya wiki
Ukatamani kukula ila chakula kooni hakipiti
Ukashindia uji na uici ya matikiti
Ukatamani kufa ili mora akuepushe na kikombe hiki
Ila ,ukasahau kuna mtu mwaka wa tano kitandani anaughulia
Maumivu zaidi ya yale unayoyapitia
Hana msaada,jamaa na ndugu wamemtenga
Anasota juu ya chaja na bado mora kumchukua hajapenda
Inaezekana ukawa umepoteza ajira kwa miezi kadhaa
Kwa maisha ukapoteza dira
Ukawa huna chochote cha kukuongezea ujira
Ukamlaumu mkesi ukamdhurumu mola hasira
Ukakosa fikira ukajiona tahira
Kuna mtu ako na miaka mitano ebu fikiria
Hajai kupata kazi ama kuitwa kwenye usaili
Anasaga soya kiatu kutafuta kazi
Na anaaminiiko siku milango itakuwa wazi
Umeshawahi kupigika na maisha haya
Uchumi ukawa kwenye hali Fulani mbaya
Ukatamaniungezaliwa mbwa ulaya
Ama uende ugaibuni kufanya kazi ya uyaya
Ulishawahi kuzitazama filamu za magharibi
Ukadhani wote walioko maisha hufaidi
Kuna ombaomba mwingi tu ughaibuni watu wasiouona
Makazi na maskini wali duni
Filamu ni mpangilio wa matukio ya kuigiza
Yanatoa nuru na kutoa giza
Ulishawahi kukumbwa na madeni kiasi kwamba
Unaona usitembelewe na wageni kwa sababu
Huna cha kuwapa zaidi ya glasi ya maji
Ulishakula faida yote ukatafuna mtaji
Ukawa unakopa mkopo ili kulipa mkopo
Ukashidwa marejesho ukafikirisiwa mali zako zilizopo
Amini wewe ni wa maana mungu hakukuumba bila sababu
0 notes