Tunapangisha Ofisi zenye fanicha zilizopo Kijitonyama; Washauri wa Ardhi, Uwekezaji, Ujenzi & Kusimamia Mradi. Real Estate Development & Management +255744112003 Join our Telegram group t.me/hamiahapatz
Don't wanna be here? Send us removal request.
Photo


















$297,500/2 br/984 sq ft
Joshua Tree, CA
built in 1967
1K notes
·
View notes
Text
KIBALI CHA UJENZI, UTARATIBU WA KUPATA, GHARAMA & MASWALI YAHUSUYO.
Kibali cha Ujenzi (Building Permit) ni nyaraka ya kisheria inayotolewa na Mamlaka za Upangaji (Planning Authorities) ambazo ni Mamlaka za Serikali za Mitaa (The Local Government Authorities) ili kuruhusu Ujenzi mpya, kubomoa, kuondosha, kuongeza, au kufanya marekebisho makubwa. Kisheria si ruhusa kwa mtu yeyote kujenga au kuanza kujenga jengo bila ya kuwa na; - Uhalali wa umiliki wa ardhi mahali unapojenga. - Kibali cha ujenzi kutoka mamlaka husika.
Katika makala hii tumegawanya vipengele vifuatavyo kwa ajili ya uelewa.
1. JINSI YA KUPATA KIBALI CHA UJENZI.
Unatakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo: - Michoro ya ramani ya jengo kwa ajili ya uchunguzi. - Risiti/Slip ya benki ya malipo stahiki ya uchunguzi wa ramani hizo. - Risiti au Slipu ya benki kwa malipo ya kiwanja kwa mwaka husika.
2. JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI MICHORO YA MAJENGO MAALUMU.
Michoro ya majengo maalumu(Maghorofa, kumbi, Taasisi mbalimbali, Bar, Vituo vya mafuta, Viwanda, Hospital na majengo mengine ya jinsi hiyo iwasilishwe kwa kuanza na michoro ya awali ya kisanifu (Preminary Drawings) ambayo itahusisha. - Michoro ya sakafu(Floor plan) 1:100 - Sura ya jengo(Elevations) 1:100 - Mkato wa jengo(Section) 1:100
Baada ya uchunguzi wa michoro ya awali kukamilika itawasilishwa michoro ya michoro (Final Drawings) ambayo ni michoro ya kisanifu na ya kihandisi(Architectural and structural drawings) kwa ajili ya uchunguzi.
● Michoro inayowasilishwa izingatie kanuni na taratibu zote muhimu za kiuchoraji(Architectural and Engineering Aspects) na iwe imesainiwa na msanifu majengo/Mhandisi anayetambuliwa(Architectural and Structural Endorsement). ● Michoro hiyo iambatane na nakala ya cheti cha uchunguzi wa athari za kimazingira(Environment Impact Assessment EIA). ● Michoro iambatane na nakala za nyaraka zote halali za umiliki wa kiwanja husika pamoja na stakabadhi ya malipo ya kiwanja kwa mwaka husika. ● Michoro yote iwasilishwe ikiwa na maandishi yanayosomeka(Readable text). ● Michoro yote iwasilishwe kwenye ukubwa wa karatasi(paper size) A0,A1,A2 au A3.
3. JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI YA MICHORO YA MAJENGO YA KAWAIDA.
Michoro ya majengo ya kawaida itawasilishwa kwa kuzingatia maelezo ya hapo juu isipokuwa haitatangulizwa na michoro ya awali (Preminary Drawing) kama ilivyo katika michoro ya majengo maalumu.
4. MICHORO ILIYOANDALIWA IONYESHE NINI?
● Jengo litakavyokuwa(Plans, Sections, Elevations, Foundation,Roof plan,Site plan). ● Ramani ya kiwanja(Location plan). ● Namba na eneo la kiwanja kilipo. ● Jina la mmilikaji ardhi inayohusika. ● Jina la mchoraji, ujuzi na anuani. ● Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba. ● Ujazo wa kiwanja(Plan ratio). ● Urefu wa jengo(Height). ● Matumizi yanayokusudiwa. ● Idadi ya maegesho yatakayokuwepo. ● Umbali kwa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja(Setbacks). ● Mfumo wa kutoa majitaka hadi kwenye mashimo.
5. VIAMBATANISHO UNAVYOTAKIWA KUWA NAVYO
● Fomu moja ya maombi iliyojazwa kwa usahihi.
● Fomu moja ya maombi iliyojazwa kwa usahihi.Hati ya kumiliki kiwanja au barua ya toleo. ● Kumbukumbu zingine zinazohusu kiwanja hicho kama hati za mauzo makabidhiano na mengine. ● Nakala ya risiti ya kodi ya kiwanja na kodi za majengo. ● Mabadiliko ya matumizi ya ardhi. ● Ramani ya kiwanja iliyosajiliwa.
6. TAHADHARI
Endapo mwananchi yeyote atajenga au kukarabati nyumba bila kibali cha ujenzi toka halmashauri, atapewa ilani ya kusimamisha ujenzi au ukarabati na kushauriwa kufuata taratibu za kuomba kibali cha ujenzi ndani ya siku 7. Kama mwombaji atakaidi ilani ya kusimamisha jiji au miji litampa ilani ya kubomoa jengo lake mwenyewe na akishindwa jiji litabomoa jengo husika na kudai mmiliki gharama za utekelezaji wa ubomoaji
....................................................................................................................
Je, uliwahi kufuatilia Kibali cha Ujenzi? Ulipitia hatua zipi na changamoto zipi? Una swali au nyongeza kuhusu Kibali cha Ujenzi? Karibu sana!
Mdau 1: Ahsante mkuu kwa mada. Hivi inachukua muda gani mpaka kupata kibali cha ujenzi?
Jibu: Ningependa kujibu kwa urefu swali hili:
Kwanza ifahamike wazi kuwa moja ya changamoto zinazokabili shughuli za Ujenzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ni pamoja na kuchelewa kutolewa kwa Vibali vya Ujenzi. Benki ya Dunia katika taarifa yake kuhusu urahisi wa kufanya biashara (Doing Business) ya Mwaka 2012 inaonesha kuwa katika kiashiria cha Vibali vya Ujenzi (Building Permits Indicator) nchini, mwombaji analazimika kupitia hatua kumi na tisa (19) na siku 303 ili kukamilisha hatua zote za maombi ya Kibali cha Ujenzi. Utaratibu huu si wa kuridhisha.
Hii ni tofauti na takwa la kisheria ambapo kwa kwa mujibu wa Kifungu cha 35 (i) cha Sheria ya Mipangomiji Na. 8 ya mwaka 2007, Mamlaka ya Upangaji inatakiwa kutoa kibali cha Ujenzi katika kipindi kisichozidi siku 60 kuanzia tarehe mwombaji alipowasilisha maombi yake. Aidha, ndani ya muda huo mamlaka inatakiwa kumjulisha mwombaji kuwa amekubaliwa au amekataliwa ombi lake na kutaja sababu zilizopelekea ombi lake kukataliwa.
Mwaka 2018 Serikali ilitoa mwongozo wa utoaji wa Vibali vya Ujenzi ambapo muda wa kukaa vikao vya kuidhinisha maombi ya Vibali vya Ujenzi umepunguzwa kutoka kufanyika kila baada ya miezi 3 mpaka (kila baada ya) wiki 2.
Kujibu swali lako sasa mkuu: Muda wa kutoa Vibali vya Ujenzi unatofautiana kutegemeana na aina ya jengo na ukubwa (complexity of the buildings) wa jengo. Ukaguzi unatakiwa kufanyika kwa umakini mkubwa. Jedwali hapa chini linaonesha muda wa kutoa Vibali kwa majengo tofauti.
Kwa ujumla ni kuwa: Endapo mwombaji atakamilisha hatua zote muhimu kwa wakati atapata kibali cha ujenzi ndani ya majuma mawili(2) hadi manne(4).Ahsante
Mdau 2: Ni sheria ipi inayosema ni lazima kuwa na kibali cha ujenzi mtu anapotaka kujenga? Kwenye post yako umesema tu 'Kisheria"…naomba tu kuelewa Dada, usinichoke.
Jibu: Hapana, siwezi kukuchoka ni wajibu wangu kuhakikisha unaelewa mada hii.
Sheria mbalimbali zimeeleza ulazima wa kuwa na Kibali cha Ujenzi.
Kwa mujibu wa Vifungu 124 na 125 vya Kanuni za Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) (Udhibiti Uendelezaji), Sura 288 (GN 242 ya mwaka 2008), Ujenzi wowote ndani ya Mamlaka za Upangaji ambazo ni Mamlaka za Miji Midogo, Halmashauri za Miji, Manispaa na Ma-jiji ni lazima upate kibali cha Ujenzi kutoka kwenye Mamlaka husika.
Mdau 3: Hivi document anayopewa mtu na mamlaka inayotoa vibali vya ujenzi baada ya kumaliza ujenzi wa jengo lake inaitwaje?
Jibu: Document inaitwa Certificate of Occupation au Cheti cha Kutumia Jengo kwa lugha ya Kiswahili.
Cheti hiki hutolewa baada ya kufanyika kwa ukaguzi wa mwisho kwenye majengo ya maghorofa na majengo makubwa na wataalam wote wahusika ili kuhakikisha kuwa miundombinu na mifumo ya majitaka, maji safi, umeme, matumizi, barabara zinakidhi vigezo. Cheti kitatolewa na Halmashauri husika baada ya kuridhika na Ujenzi ulivyokamilishwa.
Mdau 4: Kwa hiyo mtoa mada kibali cha ujenzi hupatikana serikali za mtaa au office ya serikali ya mtaa?
Jibu: Ahsante kwa swali zuri. Kwanza, tujikumbushe kuwa kuna Serikali Kuu (The Central Government) na Serikali za Mitaa (The Local Government).
Pia ni vyema kufahamu kuwa kuna mifumo miwili ya Serikali za Mitaa, mfumo wa Mamlaka za Wilaya na ule wa Mamlaka za Miji.
Kibali cha Ujenzi hupatikana katika Mamlaka za Serikali ya Mtaa(Local Government Authorities). Hapa tunazungumzia Mamlaka za Upangaji (Planning Authorities) ambazo hupatikana katika Mamlaka za Halmashauri ya Wilaya na Mamlaka ya Mji (District & Urban Authorities).
Mdau 5: Hivi unalipia bei gani kupata kibali cha ujenzi wakuu?
Jibu: Mkuu, kwanza naomba ifahamike kuwa miongoni mwa changamoto zilizokuwepo katika utaratibu wa kutoa Vibali vya Ujenzi ni kutofautiana kwa gharama baina ya Halmashauri moja na nyingine.
Ili kutatua changamoto hiyo, Mwongozo wa Utoaji Vibali vya Ujenzi uliotolewa mwaka 2018 unaeleza kuwa Halmashauri zitoze ada za aina mbili:
1. Ada ya ukaguzi (Scrutinization Fee) wa michoro ya jengo/majengo 2. Ada ya Kibali cha Ujenzi (Building Permit Fee).
Ada hizo ni “non refundable” (hazirudishwi) na znatakiwa kulipwa kwa pamoja wakati wa kuwasilisha nyaraka za maombi ya kibali cha ujenzi. Pia ada hizi zinatakiwa kuzingatia vitu vifuatavyo;
1. Ukubwa wa jengo na urefu wa jengo (Building Size and Height) 2. Matumizi ya kiwanja husika (Land Use) 3. Aina ya jengo (Type of Building)) 4. Ujazo wa kiwanja (Plot Coverage)
Kuhusu gharama halisi tuwasubiri wakuu wengine watakuja kuongezea nyama.
Mdau (Jibu): Kigamboni wana utaratibu wao, kuna sehemu nimeona hii taarifa ya 2019:
Mkurugenzi wa Kigamboni alitaja gharama za vibali vya ujenzi kwa maeneo ya makazi kuwa ni Sh 50,000 (mita za mraba 0–50), Sh 100,000 (mita za mraba 51–100) na Sh 150,000 (mita za mraba 101–150). Pia huko waliandaa michoro kwa wananchi ambao hawana uwezo wa kwenda kuchora ambapo kwa nyumba ya vyumba viwili inauzwa Sh 30,000, vitatu (70,000) na vinne (150,000).
Mdau 6: Naomba kuuliza swali la nyongeza, hiki kibali cha ujenzi kibatolewa hata kwa viwanja vya uvamiz? maana unakuta katika viwanja vya uvamizi wale wanaouzianaga 50,000 kiwanja mtu akinyanyua kichumba chake kimoja au viwili et wanakuja kuandika maandish mekundu BOMOA, FIKA SERIKALI YA MTAA…Na ukienda wanakuuliza kibali cha ujenzi pale, na wanajua kabsa ni pa uvamiz.. Hili limekaaje wakuu??
Jibu: Mamlaka za serikali hawawezi kufahamu kama anayejenga ni mmiliki halali au sio mmiliki halali wa kiwanja japo wanaweza kufahamu kama kiwanja kimemilikishwa au la. Aidha ni muhimu kabla ya kuanza ujenzi, kuwa na kibali cha ujenzi hivyo ni wajibu wao kuandika maandishi hayo. Baada ya anayejenga kufika serikali za mtaa, ndipo inaweza kujulikana kama ni mmiliki halali au la, na vivyo hivyo kuchukuliwa hatua na mmiliki halali.
Kwa ushauri wa kitaalamu zaidi, wasiliana nasi WhatsApp kwa kubonyeza hapa au kupiga namba +255744112003
Hiki ni kipeperushi cha Halmashauri ya Temeke, kikielezea zaidi juu ya kibali cha ujenzi.
#kibali cha ujenzi#gharama za kujenga#Tanzania#Dar es Salaam#Building permit in Tanzania#Building permit#building code#nyumba#ujenzi#jenga nyumba#jenga#architect#engineer#construction
0 notes
Text
JINSI YA KUFANYA MAKADIRIO YA GHARAMA ZA UJENZI WA NYUMBA YAKO - S2
SEHEMU YA PILI: MAHESABU YA IDADI YA MIFUKO YA CEMENT NA MCHANGA INAYO HITAJIKA KUJENGEA NYUMBA YAKO
Habari wana Ujenzi!, tunaendelea na muendelezo wa kufanya mahesabu ya malighafi za ujenzi. Ikumbukwe hapa tuna lenga kupanua maarifa ili kuwa na upana wa ufahamu wa mambo mbalimbali ya ujenzi kama ilivyo lengo la group hili.
youtube
Kwahiyo leo tunaingia sehemu nyingine ambayo itahusu ukadiliaji wa idadi ya mifuko ya cement itakayo hitajika kujengea jengo lako
NB: kumbuka haya huwa ni makadilio, hivyo sio lazima yawe exactly asilimia 100, lakini mara nyingi yako karibuna ukweli halisi kwa asilimia kubwa sana
Tukichukulia mfano wa TOFALI 2,000
Hapa nazungumzia tofali ambazo wengi wanaziita za block, ambazo kitaalamu zinaitwa SAND CEMENT BLOCKS
Hapa tuseme idadi ya tofali za msingi (inch 6) ni tofali 700
Idadi ya tofali za kuta (inch 5) ni tofali 1,300
A: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA MSINGI (TOFALI INCH 6)
-Ikumbukwe hapa tofali hizi hujengwa kwa kulazwa
-hivyo tofali hizi zitahitaji cement na mchanga zaidi kuliko zile za kusimama (inch 5)
KANUNI
Mfuko 1 wa cement unajenga tofali 45 za msingi (inch 6 - za kulaza)
Hivyo ukichukulia zile tofali 700 za msingi kwenye ule mfano wetu itakuwa ifuatavyo
Tofali 700 gawanya kwa 45 = 15.5 sawa na mifuko 16 ya cement
NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement unajenga tofali 50 ama 60 za msingi za kulaza) ili kupunguza gharama, lakini inamaanisha ubora unapungua pia.
B: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA KUTA (TOFALI ZA INCH 5)
-Tofali hizi mara nyingi hijengwa kwa kusimama
-Hivyo hazili mchanga na cement nyingi kama zile za msingi
KANUNI
Hapa mfuko 1 wa cement unajenga tofali 60 za kuta (inch 5- za kusimama)
Hivyo ukichukulia tofali 1,300 za kuta kwenye ule mfano wetu, itakuwa kama ifuatavyo
Tofali 1,300 gawanya kwa 60 = 21.6 sawa na mifuko 22 ya cement
NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement unajenga tofali 70 mpaka 90 za kuta, za kusimama)ili kupunguza gharama, lakini inamaanisha ubora unapungua pia.
NB: KIPIMO CHA MCHANGA
Mfuko 1 wa CEMENT una changanywa na NDOO 9 kubwa za MCHANGA
Ama mfuko 1 wa CEMENT unachanganywa na NDOO 18 ndogo za MCHANGA
MAHESABU YA IDADI YA NONDO KWA AJILI YA MSINGI NA LINTA
Kwanza ni lazima utambue kwamba NONDO zina umuhimu gani katika ujenzi wa nyumba yako.
MUINGILIANO WA NONDO NA ZEGE: nondo na zege zinatengeneza muingiliano sahihi kabisa katika ujenzi. Hii inatokana na sababu mbalimbali
- Nondo zina tabia zote yaani nguvu katika mgandamizo (compression strength)na nguvu katika uvutano (tension rate)
Zege lina nguvu kubwa ya mgandamizo (high compression strength) lakini haina nguvu kubwa ya mvutano (low/poor tension strength). Hivyo tunapo unganisha hivi vitu viwili yaani zege na nondo unapata tabia zote mbili yaani nguvu kubwa katika mgandamizo na mvutano ama mbonyeo
Ikumbukwe kwamba zege hutumika katika ujenzi wa sehemu mbalimbali katika majengo kama vile MSINGI, NGUZO, BIMU, SLABU, NGAZI, LINTA N.K
Kwahiyo sasa tunaweza kutazama umuhimu wa zege lenye nondo (Reinforced Concrete /R.C) katika ujenzi
o Ni imara, haiathiriwi na moto kiurahisi na haishambuliwi na wadudu kama ilivyo kwa mbao.
o Majengo yenye zege imara haya ruhusu maji na unyevu kiurahisi
o Inapunguza gharama za kufanya marekebisho (maintenance) mara kwa mara
o Zege lenye nondo ni rahisi kulitengeneza katika muundo wowote unao hitaji
Sasa baada ya kupata elimu kidogo na mwanga juu ya nondo na zege kwa ujumla sasa twende kwenye hesabu za namna ya kufanya mahesabu ya idadi za nondo katika jengo.
Kama kawaida yetu tutakuwa na mchoro wa msingi utakao tusaidia kufanya mahesabu (utakao tumika kama mfano).
Kwanza ni vizuri kutambua kwamba nondo zipo katika ukubwa mbalimbali
Nondo huanzia ukubwa wa kipenyo cha 8mm, 10mm, 12mm, 16mm, 20mm, 25mm na 32mm. hizi zote huwa na urefu wa 12m. (‘mm’ maana yake milimita, na ‘m’ maana yake mita
Baada ya kujua hilo, ni vema kujua pia kwa majengo ya nyumba za kawaida za kuishi huwa tunatumia sana nondo za 12mm na urefu wa 12m.
KANUNI YA KUTAFUTA IDADI YA NONDO
IDADI= JUMLA YA UREFU WA KUTA (MSINGI) GAWANYA KWA UREFU WA NONDO MOJA KISHA ZIDISHA KWA 4 AU 3
-tunazidisha kwa 4 kwasababu maranyingi nondo hizi huwekwa nne, yaani chini mbili na juu mbili zinafungwa kwenye ring yenye pembe 4
- tunazidisha kwa 3 kwasababu wakati mwingine nondo hizi huwekwa tatu, yaani chinp mbili na juu moja zinafungwa kwenye ring yenye pembe tatu
UKIANGALIA MCHORO WA HAPO JUU JUMLA YA UREFU WA KUTA (MSINGI) NI
4+2+3+4+4+2+4+2+3+4 = 32m (hii ni jumla ya kuta zote za msingi,)
Idadi = (32m/12m)4
=2.66x4
=10.6 sawa na nondo 11
Kwa wanao tumia nondo 3 basi itakuwa
Idadi = (32m/12)3
= 2.66 x 3
= 7.9 sawa na nondo 8
Kumbuka mzunguko wa msingi ni sawa na mzungo wa linta hivyo idadi ya nondo za msingi zitafanana na za linta kama utaweka zote kwa uwiano mmoja.
Ni matumaini yangu muendelezo wa makala hii utakuja uwezo na ujasiri wa kuamua kufanya makadirio ya gharama za kujenga ile nyumba ya ndoto yako.
KWA USHAURI NA MAONI wasiliana nasi WhatsApp hapa
#ujenzi#kadiria gharama ya ujenzi#gharama za ujenzi#jenga#quantity surveyor#QS#architect#architecture#gharama ya kujenga nyumba ya vyumba viwili#gharama ya kujenga nyumba ya vyumba vitatu#Dar es Salaam#Tanzania
1 note
·
View note
Text
JINSI YA KUFANYA MAKADIRIO YA GHARAMA ZA UJENZI WA NYUMBA YAKO - S1
SEHEMU YA KWANZA: MAHESABU YA IDADI YA TOFALI ZINAZO HITAJIKA KWAAJILI YA UJENZI WA MSINGI NA KUTA (TOFALI ZA BLOCK)
Habari wana Ujenzi!, nimegundua watu wengi wanapata changamoto ya kufahamu makadilio ya material wanayo hitaji katika ujenzi wa nyumba ama majengo mbalimbali. Kwasababu hiyo nimeamua kuanza mfululizo wa kutoa elimu hiyo na leo tutaanza na mahesabu ya idadi ya tofali zinazo hitajika kujenga.
youtube
Kabla haujaanza kufanya mahesabu lazima uwe na vitu vifuatavyo
1. Uwe na ramani yenye vipimo ili kujua ukubwa wa jengo lako. Ramani inachorwa na wasanifu majengo wataalamu ambao wanasomea — wataalamu hawa wanahitimu katika vyuo vinne tu hapa nchi navyo ni Ardhi University (chuo kikuu), na vyuo vya kati Ardhi Institute — Tabora, Ardhi Insitute — Morogoro, Institute of Lands Dar es Salaam.
2. Ufahamu aina ya material ama tofali utakazo tumia, kama ni hydraform, tofali za kuchoma ama blocks, hii ni kwasababu tofali zina tofautiana size ama ukubwa hivyo hata idadi yake itakuwa tofauti. Tofali zipo za aina tatu, ukubwa wake ni (length x width x thickness/urefu x upana x unene)
HYDRAFORM; 90 mm x 240 mm x 40 mm
BLOCK; 450 mm x 230 mm x 130 mm
KUCHOMA; 450 mm x 230 mm x 150 mm
Hapa tuta tumia mfano wa nyumba hii yenye vyumba viwili-kimoja kikiwa na choo/bafu ndani, sebule, jiko, choo cha wageni na vibaraza viwili; kufanya mahesabu ya tofali zetu.
Hapa kuna hatua mbili za kufuata
1. Tafuta eneo la kuta zote
2. Jumla ya eneo lote la kuta gawanya kwa ukubwa wa tofali
KUTAFUTA ENEO LA KUTA
Hapa tuta tumia kanuni ifuatayo
Eneo = Urefu( wa kuta) x kimo (urefu wa ukuta kwenda juu)
Sasa kujua urefu wa kuta zote, utatakiwa kujumlisha urefu wa kuta zote
Kwenye mchoro wetu pale juu nime weka namba kila kuta hivyo itakuwa kama ifuatavyo {vipimo vipo katika milimita (mm)}.
1 m = 100 cm = 1,000 mm; 1 cm = 10 mm
Ukuta 1= 6,500 mm; ukuta 2 = 9,150 mm; ukuta 3 = 4,000 mm; ukuta 4 = 4,000 mm; ukuta 5 = 9,450 mm
Ukuta 6=11,046 mm, ukuta 7=6196 mm +3200 mm, ukuta 8=9,101 mm, ukuta 9 =3,060 mm, ukuta 10 = 2,900 mm
Sasa uki jumlisha kuta hizo zote unapata jumla ya = 68,603 mm
Eneo la kuta = urefu wa kuta x kimo cha kuta
Hapa kama utajenga nyumba ya kozi 13 maana yake ni kimo cha 3000 mm
Hivyo eneo litakuwa = 68,603 x 3000= 205,809,000 mm
Sasa kumbuka tuna sehemu za wazi ambazo hizi hazihitaji tofali, mfano milango, madirisha na sehemu za wazi za vibaraza
Kanuni ni ile ile urefu x kimo:
Tuna madirisha 6 yenye urefu 2,000 mm & kimo 1,800 mm= 2000 x 1800 sawa na 3,600,000 mm
sasa, tuna madirisha sita yenye vipimo sawa hivyo 3,600,000 x 6 = 21,600,000
Tumia dirisha 1 lenye urefu 1,400 na kimo 1,500 = 1,400 x 1500 sawa na 2,100,000 mm
Tuna dirisha 1 lenye urefu 1,000 na kimo 1,800 = 1,000x1, 800 sawa na 1,800,000 mm
Tuna madirisha 2 yenye urefu wa 800 na kimo 600 = 800x600 sawa na 480,000 mm
480,000 zidisha kwa 2 sawa na 960,000 mm
Tuna milango 9 yenye urefu wa 900 na kimo 2,400 = 900 x 2,400 sawa na 2,160,000 mm
2,160,000 zidisha kwa 9 sawa na 19,440,000 mm
Uwazi wa vibaraza jumla uref 10,010 kimo 2,400 =10,010 x 2,400 sawa na 24,024,000 mm
Jumla ya wazi = 21,600,000 + 2,100,000 + 1,800,000 + 960,000 +19,440,000 + 24,024,000 = 69,924,000 mm
Eneo kamili linalo hitaji tofali za kuta lita kuwa
ENEO LA KUTA — ENEO LA WAZI0 = 205,809,000–69,924,000= 135,885,000 mm
hivyo basi, IDADI YA TOFALI, itakuwa kama ifuatavyo:
Sasa urefu wa msingi wako utategemea na nature ya eneo lakini tuchukulie utakuwa na urefu wa 900 mm, ambapo ni sehemu tambarare (isiyo korofi)
Kumbuka jumla ya urefu wa kuta zote ni 68,603 mm
Kwahiyo 68,603x900 = 61,742,700 mm
Kwahiyo kupata tofali tutalazimika kuchukua jumla ya ukubwa wa kuta ukiwa umetoa uwazi na jumla ya eneo la kuta za msingi kisha tuta gawanya kwa eneo la tofali moja
135,885,000+61,742,700= 197,627,700 mm
Kumbuka tofali ya block lina urefu wa 450 mm na kimo cha 230 mm
Hivyo eneo la tofali ni 450 x 230=103,500 mm
Idadi ya tofali itapatikana kwa 197,627,700mm/103,500mm = 1,909 matofali
Hapa utahitaji kuongeza asilimia kidogo ya tofali kwaajili ya zile zitakazo vunjika na ngazi pia, tutatumia 5%, kwahiyo jumla ni tafali 1909+ 0.05(1909) = 2,004.45 ≈ 2,000 tofali
MAHESABU YA IDADI YA MIFUKO YA CEMENT NA MCHANGA INAYO HITAJIKA KUJENGEA NYUMBA YAKO
hapa tunaingia sehemu nyingine ambayo itahusu ukadiliaji wa idadi ya mifuko ya cement itakayo hitajika kujengea jengo lako.
NB: kumbuka haya huwa ni makadilio, hivyo sio lazima yawe sawa kwa asilimia 100, lakini mara nyingi yanakaribia ukweli halisi kwa asilimia kubwa sana
Tukichukulia mfano wa TOFALI 2,000
Hapa nazungumzia tofali ambazo wengi wanaziita za block, ambazo kitaalamu zinaitwa SAND CEMENT BLOCKS
Hapa tuseme idadi ya tofali za Msingi (inch 6) ni tofali 700
Idadi ya tofali za kuta (inch 5) ni tofali 1300
A: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA MSINGI (TOFALI ZA INCH 6)
-Ikumbukwe hapa tofali hizi hujengwa kwa kulazwa
-hivyo tofali hizi zitahitaji cement na mchanga Zaidi kuliko zile za kusimama (inch 5)
KANUNI
Mfuko 1 wa cement unajenga tofali 45 za msingi (inch 6- za kulaza)
Hivyo ukichukulia zile tofali 700 za msingi kwenye ule mfano wetu itakuwa ifuatavyo
Tofali 700 gawanya kwa 45 = 15.5 sawa na mifuko 16 ya cement
NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement unajenga tofali 50 ama 60 za msingi za kulaza). Hii hufanywa ili kupunguza gharama japo kama ni kwenye kiwanja korofi inaweza kuleta shida.
B: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA KUTA (TOFALI ZA INCH 5)
-Tofali hizi mara nyingi hujengwa kwa kusimama hivyo hazili mchanga na cement nyingi kama zile za msingi
KANUNI
Hapa mfuko 1 wa cement unajenga tofali 60 za kuta (inch 5- za kusimama)
Hivyo ukichukulia tofali 1,300 za kuta kwenye ule mfano wetu, itakuwa kama ifuatavyo
Tofali 1,300 gawanya kwa 60 = 21.6 sawa na mifuko 22 ya cement
NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement unajenga tofali 70 mpaka 90 za kuta, za kusimama), pia hii ni ili kupunguza gharama.
NB: KIPIMO CHA MCHANGA
Mfuko 1 wa CEMENT una changanywa na NDOO 9 kubwa za MCHANGA
Ama mfuko 1 wa CEMENT unachanganywa na NDOO 18 ndogo za MCHANGA
Katika makala ijayo tutaendelea na kujumlisha gharama za usafirishaji, gharama za malighafi ya kumalizia nyumba (finishing) na nyinginezo.
Tunatoa ushauri wa kitaalam na kufanya ujenzi, usanifu majengo (ramani) & kukadiria gharama za ujenzi. Tafadhali tuandikie maoni (comment) yako hapo chini & kisha washirikishe (share) na wengine makala hii.
#ujenzi#jenga#nyumba#vyumba vitatu#makazi#gharama za ujenzi#kadiria gharama#kadiria#quantity surveyor#QS#Architect#architecture#jenga leo#nataka kujenga nyumba#kadiria gharama ya ujenzi#jinsi ya kukadiria gharama
9 notes
·
View notes
Video
youtube
Eric Kigada on the historic neglect of Nairobi and why slums do not disappear
9 notes
·
View notes
Photo

It is post your graduation day where all your relatives attended to make sure that the son/daughter of their relative is really becoming a money maker for the clan, expectations are high on you. Let’s say you have landed a dream job (only in movies) say it again? And real life is hitting on your face. You have been comfortably living with mum and dad, obeying their house rules but we know that it is not easy at all. If you’re still not sure whether you need to finally move out of your parents’ house, let’s get you sorted. Below are some obvious signs that you need to stop sharing a roof with mum and dad.
1. Privacy concerns
As a young adult, there are things you start to put away from public, even siblings – like your cellphone, laptop, personal diary, bath and body products and things of such. Even if you do want them to be known, sometimes you want them not to be used by anyone. The clothes and shoe sharing game with siblings and with mum/dad is no longer cool and personal stuff is to be at your reach only. Old habits die hard, siblings may not get this very quickly-especially those down the line and trouble will start to brew.
2. Responsible Shoulders
Learning to become accountable to oneself and others is the pinnacle of adulthood. But can it come when you are being provided for at home, freely? Experience is the best teacher they say and being on your own out there will teach you very important life skills. Having no one to turn to when faced with hardships can lead to a better citizen/individual who can ultimately rear a better family.
3. Freedom of Choice
Who does not like an independent life where you are not reliant on anybody? The life where you count more on you and less on others. You believe in your instincts more than your parents’ experience. Then be it in monetary terms or for simple household chores. Doing everything on your own imparts a confidence which is much required in the today’s tough life.
4. My House, My Rules
I feel your pain! The wahala you go through living under someone’s roof by abiding by their rules. It’s pretty natural and you can’t really blame your parents because of what they like, you might not like and what you like, they definitely don’t like. So having a place of your own gives you the freedom to design it the way you want, make your own rules, live life on your own terms and have burger for dinner for endless number of days!
5. Growth Urge
When you are on your own - dad’s not going to clean the car for you, mum’s not going to clean your disgusting bathroom and no one is going near your dirty laundry. And guess what you have to do the dishes! This will help you to grow to become a responsible young adult who can take care of themselves. Hardship makes everyone to have a clearer perspective on life.
6. End The Curfews!
The thing is your parents still worry about you. When they know you’re out, they want to make sure you get home in one piece. That can sometimes mean requesting you come home before they go to sleep. It’s easy to get angry at them when they treat you like you’re 17, but it’s sort of tough to blame them.
7. Friends Can’t Visit Anytime
Your friends want to meet up for some chit chat or a significant other wants to spend time with you, but here are some other people too who are living in that same house. We can’t chill out the way we do with parents around. And at this very moment, you wish you had been living alone in your own slap me-I slap you room/town house and have all the crazy fun you are right now missing on.
8. Nagging Games
Somehow parents are very likely to point out all the flaws in their children or indicating the unfinished chores. Why clothes are still lying on bed, why there is too much piled up stuff in your room? Parents have a say in everything we do which most of the times takes the form of lecturing, scolding or punishing. To just to avoid the lecturing and nagging, you might want to move out.
9. Locking Horns
Clashing opinions with owners of the house all the time can take a toll on you. Our parents belong to a generation which is almost twice a decade older than us. They ought to have a different mindset, different ideologies and different likes-dislikes than us. Difference in opinion often leads to ego clashes where often nobody is wrong but they just can’t agree with each other often resulting to family conflicts which are unavoidable if you and your family are living under the same roof.
10. Everyone Needs Space
Your parents could go out and enjoy romantic lunches as a couple anytime they want but now they have a family which takes the prior most position in life. They become unable to manage spending some quality time with themselves. It’s time to give them some private space so that they can enjoy life the way they want. After all it’s not just about your freedom every time. Your parents’ is as much important.
We hope the list was extensive enough to churn thoughts of moving from your family home. Now buy those moving boxes, find a small housing unit to stay, pack up and say goodbye!
1 note
·
View note